Ukame wawaathiri watu 250,000 Somaliland

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Ukame

Mashirika ya misaada yanasema watu robo ya milioni wanaathirika kutokana na ukame katika eneo lililojitangazia uhuru la Somaliland.

Mashirika hayo yanasema utapia mlo umeathiri watu vibaya hasa watoto wa chini ya miaka mitano. Watu kumi na watatu wameripotiwa kufa.

Kulingana na mashirika hayo asilimia arobaini ya mifugo imekufa kutokana na ukosefu wa maji na uhaba wa chakula.

Familia zinalazimika kuishi bila vyakula vya kutosha , kunywa maji machafu na kuhamahama kutafuta chakula.

Maeneo yalioathirika zaidi ni yale ambayo huzalisha chakula kwa kiwango kikubwa.