Al-Shabab watwaa mji kusini mwa Somalia

Al-Shabab Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wapiganaji wa al-Shabab bado ni tishio maeneo mengi kusini mwa Somalia

Wapiganaji wa al-Shabab nchini Somalia wanasema wameutwaa mjini wa Janale kusini mwa nchi hiyo ambako wanajeshi wa Muungano wa Afrika waliuawa mapema mwezi huu.

Wakazi katika mji huo walisema wanajeshi wa AU walitoroka kambi yao Alhamisi na wapiganaji wa kundi hilo la Kiislamu sasa wanaudhibiti.

Rais wa Uganda Yoweri Museveni alisema wanajeshi 19 wa Uganda waliuawa wanamgambo hao waliposhambulia kambi hiyo wiki mbili zilizopita.

Wanadiplomasia kutoka nchi za Magharibi hata hivyo wanasema wanajeshi waliouawa ni karibu 50.

Wengine 50 wanadaiwa kutojulikana waliko.