Sasa Japan inaweza kupigana nje

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Sasa Japan inaweza kupigana nje

China imeilaumu Japan kwa kukiuka katiba na kupitisha sheria za ulinzi , ambazo zitairuhusu kupeleka jeshi lake kupigana vita nchi za ng'ambo kwa mara ya kwaza kabisa tangu vimalizike vita vya pili vya dunia.

Wizara ya ulinzi nchini china inasema kuwa Japan inastahili kujifunza kutokana na historia na kulinda usalama wa majirani zake.

Marekani , uingereza na Australia , wamekaribisha mabadiliko hayo ambayo yatairuhusu Japan kutoa mchango mkubwa katika oparesheni za kimataifa za kulinda amani.