Wakamatwa baada ya Guzman kutoroka jela

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Guzman alitoroka jela mwezi Julai

Mexico imewakamata watu 13 ambao wamehusishwa na kutoroka jela kwa mlanguzi mkubwa wa madawa ya kulevya Joachim Guzman kutoka jela mwezi Julai.

Hao ni pamoja na Celina Oseguera, mratibu wa zamani wa idara ya magereza na Valentin Cardenas, aliyekuwa mkurugenzi wa gereza lenye ulinzi mkali la Altiplano.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Guzman alitoroka akitumia njia ya chini kwa chini

Guzman alitoroka jela akiptia njia ya chini kwa chini kutoka chumba chake gerezani.

Maafisa wanne wakiwemo wanachama wawili ya shiria la ujasusi walishtakiwa mwezi huu kwa kushukiwa kuhusika na kutoroka jela kwa Guzman.