Muuzaji madawa ya kulevya mtoro akamatwa Brazil

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Polis nchini Brazil wamemkamata mmoja wa walanguzi wakubwa zaidi wa madawa ya kulevya nchini humo.

Polisi nchini Brazil wamemkamata mmoja wa walanguzi wakubwa zaidi wa madawa ya kulevya nchini humo.

Mario Sergio Machado Nunes, ambaye pia anafahamika kama "O Goiano" amekuwa mafichoni tangu atoroke jela miaka miwili iliyopita.

Polisi wanasema kuwa alifanyiwa upasuaji ili kubadili umbo lake na alikuwa akitumia stakabadhi bandia.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Alikuwa kati ya watu wachache waliokuwa na uhusiano wa moja kwa moja na Pablo Escobar

Mnamo miaka ya themanini alikuwa kati ya watu wachache waliokuwa na uhusiano wa moja kwa moja na aliyekuwa mlanguzi maarufu wa madawa ya kulevya raia wa Colombia Pablo Escobar.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Kiinua mgongo cha dola milioni 5 kwa mtu yeyote atakayetoa habari zitakazopelekea kukamatwa kwa Joaquin Chapo Guzman

Amekuwa akisafirisha madawa ya kulevya kati ya Marekani Kusini na Afrika .

Guianio alikamatwa akiwa katika jumba moja la kifahari katika mji wa pwani wa Guajura.

Hapo jana, maafisa wa kupambana na mihadarati walitangaza kiinua mgongo cha dola milioni 5 kwa mtu yeyote atakayetoa habari zitakazopelekea kukamatwa kwa kiongozi wa genge la wauazaji mihadarati Joaquin Chapo Guzman ambaye kama Goiano alitoroka gerezani.