Mapambano yazuka upya Burkina Faso

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mapambano yamezuka kwenye hoteli katika mji mkuu wa Burkina Faso, Ouagadougou, ambako mazungumzo ya amani yamekuwa yakifanyika, baada ya mapinduzi ya juma lilopita.

Mapambano yamezuka kwenye hoteli katika mji mkuu wa Burkina Faso, Ouagadougou, ambako mazungumzo ya amani yamekuwa yakifanyika, baada ya mapinduzi ya juma lilopita.

Wafuasi kama 50 wa kikosi cha kumlinda rais, ambacho kiliipindua serikali ya mpito Alhamisi, kiliingia kwa nguvu katika ukumbi wa hoteli, na kujeruhi waandishi wa habari kadhaa.

Image caption Haijabainika hadi kufikia sasa kiongozi wa mapinduzi haya atatoa masharti yepi ya kurejesha mamlaka kwa rais Kafondo na utawala wake.

Wapatanishi kutoka nchi za Afrika Magharibi, ambao wamekuwa wakizungumza na viongozi wa mapinduzi hayo, waligusia kuwa wanakaribia kurejesha madaraka kwa serikali ya kiraia.

Watu kama 10 wameuwawa na zaidi ya 100 kujeruhiwa katika mapambano baina ya wanajeshi na waandamanaji katika siku chache zilizopita.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wafuasi kama 50 wa kikosi cha kumlinda rais, ambacho kiliipindua serikali ya mpito Alhamisi, kiliingia kwa nguvu katika ukumbi wa hoteli

Mapambano hayo yametilia shaka tangazo la awali la Rais wa Benin, Yayi Bon, aliyesema kwa kuna uwezekano mkubwa kuwa viongozi wa wa mapinduzi hayo wako tayari kumuachilia rais Michel Kafando kutoka kizuizi cha nyumbani na kumrudish mamlakani.

Mazungumzo yamekuwa yakifanyika katika mji mkuu Ouagadougou baada ya siku ya tatu ya maandamano ya kupinga mapinduzi ya rais Kafando yaliyofanywa na kikosi cha kumlinda rais.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Waandamanaji wanamtaka rais wa kipindi cha mpwito Kafondo kurejeshwa madarakani

Akiongea na kiongozi wa mapinduzi hayo, jenerali Gilbert Diendere, rais wa Benin anasema kuwa anatarajia kile alichokitaja kuwa habari njema kutangazwa baadaye leo Jumapili.

Waandamanaji wanamtaka rais wa kipindi cha mpwito Kafondo kuendelea kushikilia hatamu hadi pale uchaguzi uliopangwa kufanyika mwezi Oktoba utakapomalizika.

Haijabainika hadi kufikia sasa kiongozi wa mapinduzi haya atatoa masharti yepi ya kurejesha mamlaka kwa rais Kafondo na utawala wake.