Canada itapokea wahamiaji 10,000

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Canada itapokea wahamiaji 10,000

Serikali ya Canada inasema kuwa haiwezi kukubali zaidi ya wakimbizi 10,000 kutoka nchini syria jinsi ilikuwa imehidi awali.

Wazir wa uhamiaji Chris Alexander anasema kuwa serikali itafanya kazi kuhakikisha kuwa zoezi la kusajiliwa kwa wakimbizi hao limefanyika ndani ya kipindi cha miezi sita.

Amesema kuwa maelfu ya wasyria huenda wakawasili nchini Canada ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Austria na Ujerumani zilitoa wito kwa wanachama wa umoja wa mataifa kutoa mchango wa zaidi ya dola bilioni tano u nusu kusaidia wakimbizi wanaoishi kambini nchini Lebanon na Jordan.

Mapema Austria na Ujerumani zilitoa wito kwa wanachama wa umoja wa mataifa kutoa mchango wa zaidi ya dola bilioni tano u nusu kusaidia wakimbizi wanaoishi kambini nchini Lebanon na Jordan.

Naibu chansela wa ujerumani Sigmar Gabriea anasema kuwa msaada unastahili kutolewa kwa nchi ambazo zinakumbwa na matatizo makubwa ambapo wahamiaji walikuwa na mipango ya kusafiri kwa miguu kwenda ulaya.