Carson:Mwislamu hafai kuongoza Marekani

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Carson:Musilamu hafai kuwa rais wa Marekani

Mmoja wa wanasiasa wanaowania kuchaguliwa kugombea urais kwa niaba ya chama cha Republican, nchini Marekani amesema Uislamu hauambatani na katiba ya taifa hilo.

Ben Carson, ambaye ni, daktari wa neva aliyestaafu, amesema yeye katu hawezi kukubali Mwislamu kuwa rais wa Marekani.

Akijibu maswali katika kipindi cha mahojiano cha runinga ya NBC ''Meet the Press, Carson anasema kuwa dini hiyo inakinzana na katiba ya Marekani.

Kura ya maoni inaonesha kuwa daktari huyo ambaye ni mkristo anashikilia nafasi ya pili kwa umaarufu nyuma ya bilionea mbishi Donald Trump.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption ''Uislamu unakinzana na katiba ya Marekani' Carson

Matamshi yake yanatokea siku chache, baada ya mgombea anayepigiwa upatu kutwaa tikiti ya chama cha Republican, Donald Trump, kukataa kujitenga na mfuasi wake, ambaye alimshutumu Rais Obama kuwa Mwislamu, na hata sio Mmarekani.