Papa Francis kuongoza misa Cuba

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Papa Francis kuongoza misa Cuba

Maelfu ya waumini wa kanisa katoliki wanahudhuria misa mjini Havana hii leo ambayo itaongozwa na kiongozi wa kanisa katoliki papa Francis ambaye anafanya ziara nchini humo kwa mara ya kwanza.

Papa Francis amezitaka Marekani na Cuba kuendelea kuboresha uhusiano kati yao.

Haki miliki ya picha epa
Image caption Papa Francis amezitaka Marekani na Cuba kuendelea kuboresha uhusiano kati yao

Akiongea kwenye uwanja wa ndege wa Havana anapoanza ziara nchini Cuba na Marekani, papa Francis alipongeza uhusiano ambao umeshuhudiwa kati ya nchi hizo.

Haki miliki ya picha REUTERS
Image caption Rais wa Cuba Raul Castro amemshukuru papa Francis kwa jitihada zake kurejesha uhusiano kati ya Cuba na Marekani

Akijibu hayo rais wa Cuba Raul Castro amemshukuru papa kwa wajibu wake katika kusaidia kurejesha uhusiano kati ya Cuba na Marekani.

Hii ndiyo ziara ya kwanza anayofanya papa Francis nchini Cuba baada ya kulakiwa na umati uliokuwa ukipeperusha bendera za Cuba wakati msafara wake ulikuwa ukipita katika mitaa ya mji wa Havana.