Azikwa akiwa hai India

Image caption Changarawe

Mtu mmoja nchini India amefariki baada ya wafanyikazi wa ujenzi ambao hawakumuona katika shimo kumzika akiwa hai.

Kisa hicho kilitokea katika wilaya ya Katani katika mji wa jimbo la Pradesh.

Maafisa wa polisi wameiambia BBC kwamba mtu huyo mwenye umri wa miaka 45 alikuwa amelewa alipoangukakatika shimo hilo.

Watu wawili akiwemo dereva mmoja wa lori ambaye alimwaya changarawe hiyo wamekamatwa.

Kisa hicho kilibainika baada ya wanakijiji kuona mkono uliokuwa umejitokeza chini ya changarawe hiyo.

Mtu huyo anaaminika kuelekea nyumbani kutoka kijiji kimoja kabla ya kuanguka katika shimo hilo.

Mamlaka ya taifa hilo imeagiza kufanyika kwa uchunguzi na kuahidi kuchukua hatua kali dhidi ya wale watakaopatikana na hatia.