Maoni ya Facebook yamtia mashakani

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Facebook

Mahakama ya Singapore imemuhukumu muuguzi mmoja kutoka nchini Ufilipino kifungo cha miezi minne kwa kuchapisha maoni ya uchochezi kuhusu taifa hilo kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook.

Ello Ed Mundsel Bello ambaye amekuwa akifanya kazi nchini Singapore aliandika kwamba raia wa taifa hilo hawako huru.

Alishtakiwa kwa kuwa muhaini na kuwadanganya maafisa wa polisi.

Akitoa hukumu hiyo jaji huyo alisema kuwa mahakama hiyo haikuweza kupuuza tishio la maoni hayo kwa jamii ilio tulivu.

Singapore ni taifa lenye raia wa mataifa na rangi mbali mbali na mamlaka hujali sana maoni ambayo yanaweza kuchochea wasiwasi wa kibaguzi.