Mtandao wa Skype wakumbwa na tatizo

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Skype

Tatizo la kimitambo limesababisha watu wengi kukosa kutumia huduma ya mtandao wa Skype.Ripoti kuhusu Skype kukumbwa na hitilafu zilianza mwendo wa saa tano za Afrika mashariki nchini Uingereza.

Katika taarifa yake,mmiliki wa Skype Microsoft amesema kuwa waligundua tatizo katika mitambo ya huduma hiyo ambayo inaonyesha iwapo kuna mtu anatumia huduma hiyo au la.

Tatizo hilo liliwazuia wanaotumia mtandao huo na hivyobasi kutoweza kupiga simu licha ya kwamba wapo mtandaoni.

Vilevile,Microsoft imesema kuwa majina ya wanaotumia huduma hiyo ambao wameathiriwa yanaonyesha kwamba hawako katika mtandao na hivyobasi kutoweza kuwapigia simu.

Wateja wengi wa Skype kutoka nchini Uingereza,Australia na Japan wameripoti tatizo hilo.

Maafisa wa mtandao huo wamekiri kuwepo kwa tatizo hilo na kusema kuwa wanafanya kila njia kutatua tatizo hilo.