Somalia:Bomu lawauwa 6 katika makao ya rais

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Bomu

Bomu lililotegwa ndani ya gari limelipuka karibu na lango kuu la jumba la rais katika mji mkuu wa Mogadishu.

Takriban watu sita wamefariki,ikiwemo walinzi wa rais.Raia mmoja wa Uturuki pia aliuawa.

Wengine 10 waliripotiwa kujeruhiwa.

Mkutano kuhusu hali ya baadaye ya uchaguzi nchini humo umekuwa ukiendelea katika jumba hilo,lakini ulikuwa umeisha wakati wa mlipuko huo.

Wajumbe wengi waliripotiwa kuondoka katika eneo la jumba hilo.

Hoteli moja karibu na jumba hilo iliharibiwa.