Ecowas kuitembelea Burkina Faso

Image caption Jeneral Gilbert Diendere

Viongozi wa mataifa sita ya Afrika Jumatano hii wataitembelea Burkina Faso kuweza kurejesha tena serikali ya mpito.

Nigeria, Togo, Senegal na Benin ni baadhi ya nchi ambazo viongozi wake wanatarajiwa kuwepo katika ziara hiyo.

Uamuzi huo umefikiwa katika kikao cha dharura cha viongozi wa nchi wa Jumuia ya kiuchumi ya nchi za Afrika magharibi ECOWAS, waliokutana nchini Nigeria.

Katika hatua ya mapinduzi Viongozi hao waliyalaani mapinduzi yaliyofanywa nchini humoi na kuwataka viongozi wake kujisalimisha bila ya masharti yoyote.

Kiongozi wa mapinduzi hayo, ambaye ameomba msamaha kwa wale wote waliopanga mapinduzi hayo awali na kusema kuwa anasubiri matokeo ya mkutano huo wa viongozi wa ECOWAS.