Afisa wa juu jela kwa rushwa:Brazil

Mahakama kuu nchini Brazil imemhukumu kwenda jela miaka 15 aliyekuwa mkuu wa idara ya fedha wa chama cha wafanyakazi,kufuatia kumbaini na makosa ya Rushwa na Ufisadi.

Joao Vaccari Neto ambaye amekumbwa na hukumu hiyo ni mtu wa karibu sana na Rais Dilma Rousseff ambaye ni kwanza kukumbwa na mkasa kama huo.

Mwendesha mashtaka nchini humo amesema kuwa kwa miaka mingi makampuni makubwa ya ujenzi yalikuwa yakitoa rushwa kwa wanasiasa na maofisa waandamizi kwa lengo ili kulinda mikataba ya kifisadi.

Hatua hiyo ya kimahakama nchini humo imeleta kashfa pia kwa Rais Rousseff kuhusishwa na ufisadi huo japo kuwa,mwendesha mashtaka anasema hakuna ushahidi wa moja kwa moja.