Masaibu ya VolksWagen yaongezeka

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Korea Kusini imetoa ilani ya kufanya uchunguzi upya kuhusiana na magari yote yanayotengenezwa na kampuni hiyo ya VolksWagen

Kufuatia ufichuzi kuwa kampuni ya kijerumani ya kutengeneza magari VolksWagen ilitoa habari ghushi juu ya utoaji wake wa gesi hatari kwa mazingira, serikali ya Marekani

sasa imesema kuwa iatafanyia uchunguzi upya magari yote yanayotumia mafuta aina ya diesel kutoka kwa watengenezaji magari yote.

Shirika la kuhifadhi mazingira la California nchini Marekani limesema kuwa linataka kujua iwapo kuna uwezekano makampuni mengine pia yaliezeka kifaa cha kubadili

matokeo wakati wa kufanyiwa uchunguzi.

Waziri wa uchumi nchini Ujerumani Sigmar Gabriel amesema kuwa anhofia kashfa hii itaichafulia jina kabisa sekta ya utengenezaji wa magari nchini Ujerumani.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Masaibu ya VolksWagen yaongezeka

Maafisa wa ngazi za juu katika kampuni ya VolksWagen wanakumbwa na shinikizo zaidi baada ya kampuni hiyo kupoteza mabilioni ya dola za hisa zake hapo jana.

Wakati huohuo, Korea Kusini imetoa ilani ya kufanya uchunguzi upya kuhusiana na magari yote yanayotengenezwa na kampuni hiyo ya VolksWagen kufuatia ufichuzi huo huko Marekani.

Serikali ya Seoul imesema kuwa inapanga kufanyia uchunguzi upya magari 5,000 ya kampuni hiyo ya VolksWagen ikiwemo yenye nembo ya VW Jetta, VolksWagen Golf Magari ya Audi A3 yaliyotengezwa kati ya mwaka wa 2014 na 2015.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Afisa mkuu mtendaji wa kampuni hiyo Martin Winterkorn ameomba radhi.

Maafisa wa serikali wanatarajia kutoa matokeo ya uchunguzi huo mwisho wa mwezi Novemba.

Tayari kampuni ya Volkswagen imeagiza wamiliki wa magari 500,000 nchini Marekani wayaregeshe viwandani iliyakafanyiwe ukarabati.

Kampuni hiyo inatarajiwa kupigwa faini kubwa ya takriban dola bilioni 18 hata baada ya afisa mkuu mtendaji wa kampuni hiyo Martin Winterkorn kuomba radhi.