Vazi la Burqa ladaiwa kuwa la itikadi kali

Haki miliki ya picha
Image caption Burqa

Mwanachama mwandamizi wa chama cha kikomyunisti katika jimbo la Xinjiang amesema kuwa vazi la kufunika uso la Burqa sio la Kiislamu bali ni la itikadi kali.

Afisa huyo alitoa matamshi yake katika hafla ya maendeleo katika jimbo hilo,ambalo ni makaazi ya Waislamu wasio wengi wa kabila la Uighur.

Serikali imeweka marufuku ya nguo za kidini katika jimbo la Xinjiang, ambapo inalaumu waislamu wanaotaka kujitenga kwa ghasia zilizosababisha vifo vya watu wengi katika kipindi cha miaka michache iliopita.