Papa akumbusha makasisi waliodhalilisha

Haki miliki ya picha
Image caption Papa Francis akiwa Washington Marekani

Papa Francis amehutubia maaaskofu huko nchini Marekani katika siku ya pili ya ziara yake na kuwasifu kwa jinsi walivyokabiliana na kashfa ya udhalilishaji wa kimapenzi inayowakabili makasisi takriban miaka kumi iliyopita.

Hata hivyo mwandishi wa BBC anaseama kitendo cha papa huyo kuacha kuwatembelea waathirika waliofanyiwa vitendo hivyo huenda kikawauzunisha baadhi ya wakatoliki.

Papa alifanya ibada ya kipapa kwa mara ya kwanza katika ardhi ya Marekani.

Mapema papa alitoa wito kufanyika hatua kukabilina na tatizo la mabadiliko ya tabia ya nchi.

Akiwa katika ikulu ya white house papa alisema suala la mapambano dhidi ya mabadililko ya tabia ya nchi lisiachiwe vizazi vijavyo.

Maelefu ya wamarekani walijipanga njiani kumlaki wakati alipokuwa akitoka ndani ya ikulu ya White House ambapo wangine walitumia simu zao za mkononi kupata picha za kumbukumbu.