Ahudumia miaka 20 jela bila hatia Uganda

Image caption Mpagi Edward Edmary

Mnamo mwaka 1982 Mpagi Edward Edmary ,dereva wa texi nchini Uganda alipewa hukumu ya kifo kwa mauaji ya kinyama ya jirani yake.

Licha ya Edward kuwa mtu asiye na hatia hakuhukumiwa na mauaji yoyote.

Edward alisingiziwa katika mgogoro wa shamba wa familia.

Mashahidi walihongwa ili kusema kuwa walimuona akimuua mtu huyo kabla ya mwili wake kuuzika.

Alitumikia kifungo cha miaka 20 katika jela ya Luziri mjini kampala na aliwachiliwa tu baada ya familia yake kubaini kwamba mtu aliyedaiwa kuuawa alikuwa mafichoni katika eneo jingine la taifa hilo.