Volkswagen zapigwa marufuku Uswizi

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Gari la Volkswagen

Taifa la Uswizi limepiga marufuku kuuzwa kwa magari aina ya Volkswagen ambayo yana mitambo ya iliyotengenezwa kudanganya majaribio ya gesi chafu.

Idara inayosimamia usafiri wa barabarani nchini humo inasema kuwa hadi magari 180,000 yataathiriwa.

Hilo ndilo pigo la hivi punde kwa kampuni hiyo ya Ujerumani tangu ikiri kuwa magari milioni 11 yanayotumia mafuta ya diesel kote duniani yamewekwa mitambo inayuweza kudanganya kuhusu gesi chafu.

Mauzo ya hisa za kampuni ya Volkswagen yameshuka katika kipindi cha wiki moja tangu kufichuliwa kwa sakata hiyo.

Mkurugenzi mpya wa kampuni ya Volkswagen amesema kuwa uchunguzi ulio wa kina na wazi utafanyika.