Watu 20 wauawa katika mapigano Bangui

Haki miliki ya picha
Image caption Watu 20 wameripotiwa kufariki kufuatia mapigano makali yaliyoibuka mjini Bangui katika jamhuri ya Afrika ya Kati.

Watu 20 wameripotiwa kufariki kufuatia mapigano makali yaliyoibuka mjini Bangui katika jamhuri ya Afrika ya Kati.

Daktari mmoja wa jeshi ameiambia shirika la habari la AFP kuwa zaidi ya watu 100 walijeruhiwa katika makabiliano baina ya waislamu na wakristu katika eneo la PK-5.

Makabiliano hayo yalitibuka baada ya mauaji ya mwendesha bodaboda ambaye alikuwa ni muislamu.

Eneo hilo la PK-5 ndilo lililokuwa chimbuko la mapaigano ya wenyewe kwa wenye kati ya waislamu na wakristu kati ya mwaka wa 2013- 2014.

Maafisa wa kijeshi wa umoja wa mataifa walioko huko walilazimika kuingilia kati ilikukomesha maafa zaidi.

Haki miliki ya picha
Image caption Wenyeji wa Bangui wameanza kutoroka makwao

Serikali ya mpwito imekashifu mauaji hayo iliyoyataja kuwa ya kipuuzi.

Taifa hilo limekuwa likijaribu kurejea katika uongozi wa kiraia na wa amani kufuatia vita vilivyotokea baada ya kundi la waasi wa Seleka ambao wengi wao ni Waislamu walipoipindua serikali ya Francois Bozize inayoungwa mkono na makundi ya wakristu ya "anti-balaka".

Kwa sasa makundi ya wakristu "anti-balaka" yanadhaniwa kushiriki katika mapigano hayo ya kulipiza kisasi na kuna hofu kubwa kuwa huenda kukaibuka mapigano zaidi.