Rihanna; Chris Brown ataingia Australia ?

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Brown ameonywa kuwa huenda asipewe ruhusa ya kuingia Australia kutokana na rekodi yake ya kumpiga mpenzi wake

Mwanamuziki wa kizazi kipya kutoka Marekani,Chris Brown ameonywa kuwa huenda asipewe ruhusa ya kuingia Australia kutokana na rekodi yake ya kumpiga mpenzi wake.

Brown alikuwa ananuia kwenda kuwatumbuiza mashabiki wake nchini humo mwezi December.

Mwanamuziki huyo ana siku 28 za kukata rufaa kwa afisi ya uhamiaji ya Australia.

Tiketi za shoo hiyo zilikuwa zimeratibiwa kuanza kuuzwa jumatatu (kesho).

Masaibu ya Chris Brown yanatokana na ripoti zilizochapishwa kote duniani mwaka wa 2009, kuwa alikuwa amemuzaba makonde mpenzi wake wakati huo Rihanna.

Japo amezuru taifa hilo mara mbili, shinikizo limejitokeza kwa serikali ta Australia kumnyima idhini ya kuingia.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Masaibu ya Chris Brown yanatokana na ripoti zilizochapishwa kote duniani mwaka wa 2009, kuwa alikuwa amemuzaba makonde mpenzi wake wakati huo Rihanna

Akitoa ilani ya kumnyima visa waziri wa uhamiaji wa Australia Peter Dutton alisema kuwa

''watu wanapaswa kufahamu kuwa mataifa mengine yanazingatia haki za wanawake kwa umakini na iwapo umewadhulumu wanyonge basi sharti ufahamu kuwa mataifa mengine yatakuadhibu''

Waziri wa maswala ya wanawake wa Australia Michaelia Cash,ambaye alikuwa naibu waziri wa uhamiaji hadi majuzi alisema kuwa waziri Dutton anapaswa kuvalia njuga swala la cheti cha kumruhusu brown kuingia Australia.

''Yafaa afahamu kuwa humu huwezi kuingia ilhali wewe huheshimu na kuwalinda watu wanyonge ikiwemo wanawake''

Haki miliki ya picha Getty
Image caption New Zealand tayari imemnyima hati ya kuingia nchini humo kwa tuhuma hizo.

Wadau hata hivyo wanasema kuwa huenda hali imekuwa ngumu zaidi kwa Brown kufuatia kauli ya kumnyima bondia maarufu wa Marekani Floyd Mayweather ruhusa ya kuingia nchini humo mapema mwaka huu.

New Zealand tayari imemnyima hati ya kuingia nchini humo kwa tuhuma hizo.