Lewis Hamilton ashinda langalanga Japan

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Lewis Hamilton ashinda mbio za magari ya langalanga ya Japan Grand Prix.

Lewis Hamilton amejitetea baada ya kumpiku dereva mwenza wa Mercedes Nico Rosberg kwenye kona hatari katika mbio za magari ya langalanga ya Japan Grand Prix.

Kufuatia hatua hiyo ya Hamilton dereva mjerumani Rosberg alilazimika kuondoka barabarani ilikuepuka wasigongane.

Rosberg alipitwa na madereva wawili wengine kabla yake kuudhibiti usukani wake tena na kurejea barabarani.

''kwa hakika sikutegemea kuwa alikuwa na uwezo wa kunizuia nisimpite katika upande wa kushoto.''alisema Hamilton.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Hamilton alimpiku mpinzani wake kwenye kona hatari

Rosberg kwa upande wake alisema kuwa alilazimika kuepuka kumgonga dereva mwenza : "nililazimika kufunga breki na hiyo ikawapa wapinzani wangu fursa ya kunipita''Kufuatia hatua hiyo Hamilton alifululiza hadi kwenye utepe na akaibuka mshindi.

Muingereza sasa anashilia nafasi ya kwanza katika jedwali la madereva bora msimu huu kwa zaidi ya alama 48 dhidi ya mpinzani wake wa karibu Rosberg.

Vilevile ushindi huu umemuwezesha Hamilton kutoshana nguvu na dereva aliyeshinda mashindano mengi zaidi duniani naye ni Ayrton Senna aliyeshinda mashindano 41 ya mbio za magari ya langalanga.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Rosberg na Hamilton walionywa dhidi ya kupalia chuki baina yao

Mwaka uliopita ushindani mkali kati ya madereva hao wenza Rosberg na Hamilton ulipelekea wamiliki wa magari ya Mercedes kuwaonya dhidi ya kupalia chuki baina yao kugongana na kuzuia mmoja wao asiibuke mshindi.

Kwa ufupi Mercedes iliwakumbusha kuwa mbali na ushindani wa kibinafsi watengenezaji magari Mercedes nao wako mbioni kutawazwa mabingwa wa kiufundi.