1 kati ya watoto 2 wanaozaliwa ni wanaharamu

Haki miliki ya picha GETTY
Image caption Je ndoa imepoteza hadhi yake?

Je ndoa imepoteza hadhi yake?

Watoto waliozaliwa nje ya ndoa walikuwa wanatambulika kama wana haramu.

Lakini takwimu za hivi punde zinaonesha kuwa mtazamo huo umebadilika kadri walimwengu wanavyoendelea kukubali maisha ya kisasa.

Takwimu za hivi punde nchini Uingereza zinaonyesha kuwa mmoja kati ya watoto wawili wanaozaliwa Uskochi Kaskazini mwa Uingereza ni vizazi vya kina mama ambao hawajaolewa na baba za watoto wao.

Hii ni kumaanisha kuwa asilimia 50% ya wanawake wanaojifungua hawajafunga ndoa.

Katika maeneo ya Kaskazini mwa Uingereza asilimia 60 ya wanawake wanaojifungua watoto wao hawajafunga ndoa.

Aidha asilimia 60% ya watu wanawekana kinyumba;hawana vyeti vya ndoa.

Kwengine katika muungano wa mataifa ya Uingereza asilimia 50 ya watu wanasusia kufunga ndoa kihalali.

Katika miaka ya 1940, asilimia 94 ya watoto wote walikuwa wanazaliwa ndani ya ndoa.

Haki miliki ya picha THINKSTOCK
Image caption Asilimia 50% ya wanawake wanaojifungua hawajafunga ndoa halali

Kwa mujibu wa idara ya utafiti wa taifa, idadi hiyo ya juu inaelekea kutoshana na ile ya mataifa ya bara Uropa kama vile Ufaransa ambapo asilimia kubwa ya watoto wanaozaliwa huko hawako katika familia za kudumu.

Takwimu hii inasadifiana na ile ya mataifa kusini mwa Marekani ambapo watafiti wamekuwa wakilaumu kuongezeka maradufu kwa mimba za mapema hususan katika maeneo yenye idadi kubwa ya umasikini katika jamii na uhaba wa ajira na kitega uchumi.

Kimsingi,wataalamu wa maswala ya jamii katika mataifa ya Marekani ya Kati wamekuwa wakitafiti uhusiano kati ya idadi kubwa ya mimba na watoto wanaozaliwa nje ya ndoa na umasikini.

Aidha kuna uhusiano mkubwa kati ya idadi kubwa ya mimba za mapema na watoto wanaozaliwa nje ya ndoa.

Utafiti huo umebaini kuwa asilimia, 72% ya watoto wanaozaliwa miongoni mwa wamarekani weusi ni wanaharamu.

Haki miliki ya picha GETTY
Image caption Asili mia 17% ya watoto wanaozaliwa miongoni mwa jamii ya wahindi wanazaliwa nje ya ndoa.

Miongoni mwa wamarekani weupe idadi hiyo ni asilimia 29% pekee.

Hata hivyo Idadi ya watoto wanaozaliwa nje ya ndoa miongoni mwa wamarekani waliochanganya asili ni 66%.

Asili mia 17% ya watoto wanaozaliwa miongoni mwa jamii ya Wahindi wanazaliwa nje ya ndoa.

Takwimu hii ni kwa mujibu wa utafiti wa mwaka huu 2015 Child Trends Databank.

Kutokana na hali ngumu ya maisha na idadi kubwa ya vijana ambao hawana kazi mahitaji ya ndoa yamezidi makadirio yao ya kifedha hivyo wanaona afadhali kuishi kinyumba tu pasi na ndoa rasmi.

Image caption Je mtoto asiye na babake anapokelewa kivipi na jamii ?

Je nini kinachangia idadi hiyo kubwa ya ndoa bandia ?

Utafiti huu bado unaendelea lakini sababu kuu ni kiuchumi.

Duniani pia kuna mabadiliko makubwa ya maadili.

Wapenzi ya jinsia moja.

Duniani kote kunaongezeko maradufu la idadi ya wapenzi wa jinsia moja wenye watoto wanao wekana kinyumba kwa sababu hawaruhusiwi kuona kihalali katika mataifa mengi.

''Wajua kuwa ukimwona mwanamke ameamua kupata mtoto akiwa nje ya ndoa hainamiishi kuwa yuko pekee yake ''asema Gretchen Livingston, mtafiti katika kituo cha utafiti wa familia cha Pew Research Center.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Je mtoto asiye na babake anapokelewa kivipi na jamii ?

Hoja yake inatiliwa pondo na matokeo ya utafiti unaoonyesha kuwa asilimia 60% ya wanawake wanaojifungua watoto nje ya ndoa nchini Marekani kwa hakika huwa na wapenzi wao ila hawajafunga ndoa.

Idadi hiyo inasemekana kuwa juu zaidi katika eneo la Latin America na katika mataifa yaliyoko Ulaya Magharibi.

Kwa mujibu wa utafiti wa asili ya familia 'The World Family Map 2014' inayothaminiwa na taasisi ya Social Trends na vyuo vikuu kadhaa

Asilimia kubwa ya watu waliohitimu umri wa kuoa na kuolewa kati ya miaka (18- 49) wana nafasi nzuri ya kufunga ndoa wakiwa barani Asia na mashariki ya kati.

Kwanini ?

Kwa sababu katika mataifa ya Asia na mashariki ya kati watu wanaheshimu mila na desturi zao.

Idadi hiyo ni tofauti sana katika mataifa ya Magharibi mwa bara Ulaya na mataifa ya Marekani ya Kati ambapo watu wameasi mila na desturi zao.

Haki miliki ya picha Tara Ruby Photography
Image caption Je katika taifa lako jamii inachukuliaje familia ya mwanamke asiye na mume ?

Katika maeneo hayo mmoja kati ya watoto wawili wanaozaliwa mmoja huwa ni mwanaharamu.

Je, katika taifa lako jamii inachukuliaje familia ya mwanamke asiye na mume ?

Je, mtoto asiye na babake anapokelewa kivipi na jamii ?

Katika mataifa tisa yaliyoko Marekani ya kati idadi ya watoto hao ni kubwa mno.

Asili mia 50% ya watoto wanaozaliwa huko ni "wanaharamu".

“katika mataifa mengi barani ulaya umri wa mwanamke anapojifungua mtoto wake wa kwanza umeshuka sana kulingana na uwezo wa kiuchumi '' “Doing Better for Families.”

Afrika

Katika bara la Afrika, idadi ya wanawake wanaojifungua nje ya ndoa ni ya chini mno nchini Nigeria ( 6% tu )

Idadi hiyo hata hivyo ni maradufu nchini Afrika Kusini (63%).

Hii inafikiriwa kusababishwa na kuimarika au kudorora kwa uchumi mila na desturi na misimamo ya kidini.

Hali inayojirejelea katika mataifa yote haya yaliyofanyiwa utafiti ni kuwa wanawake wenye umri wa miaka 20 wanazidi kupata ujauzito pasi na kuwa na wapenzi halali.

Ishara ya kuwa katika kizazi kijacho hali hii huenda ikawa kubwa zaidi.