Mwanawe Paul Walker aishtaki Porsche

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mwanawe Paul Walker wa Fast & Furious aishtaki Porsche kwa kifo cha babake

Mwanawe marehemu msanii nguli wa 'Fast and Furious'' Paul Walker ameishtaki kampuni ya kutengeneza magari ya Porsche kufuatia ajali iliyokatiza maisha ya babake.

Meadow Walker,mwenye umri wa miaka 16 anailaumu Porsche kwa kifo cha babake ambaye aliteketea hadi kufa baada ya gari alimokuwa akisafiria kugonga taa ya barabarani na kuwaka moto Novemba mwaka 2013.

Idara ya mahakama ya Marekani imethibitisha kuwa kesi hiyo imesajiliwa.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Meadow Walker,mwenye umri wa miaka 16 anailaumu Porsche kwa kifo cha babake ambaye aliteketea hadi kufa

Meadow anasema kuwa Porsche haikuzingatia usalama wa madereva na abiria ilipokuwa ikiunda mfumo wa usalama wa magari yake dhidi ya ajali.

Kampuni hiyo ya Porsche haijajibu mashtaka hayo yanayoikabili.

Uchunguzi wa Polisi uliotolewa baada ya miezi minne ulibaini kuwa gari hilo aina ya Porsche Carrera GT, lililokuwa likiendeshwa na na rafiki wa karibu wa marehemu Roger Rodas, lilikuwa likiendeshwa kwa kasi mno kilomita 151 kwa saa.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Msingi wa kesi hiyo unatokana na ushahidi kuwa gari hilo lilikuwa likienda kwa kasi ya chini ilipopoteza mwelekeo na kugonga taa kwa mujibu wa jarida la TMZ.

Eneo ilikotokea ajali hiyo haipaswi kuzidi kasi ya kilomita 72 kwa saa.

Msingi wa kesi hiyo unatokana na ushahidi kuwa gari hilo lilikuwa likienda kwa kasi ya chini ilipopoteza mwelekeo na kugonga taa kwa mujibu wa jarida la TMZ.

Jarida hilo linasema kuwa ukanda wa abiria ulimkata utumbo nyota huyo mbali na kuvunjavunja mbavu zake na kwa hivyo hangeweza kujinasua gari lilipowaka moto.

Mkewe dereva wa gari hilo Rodas aliwasilisha kesi kama hiyo mahakamani mwaka uliopita ila Porshe ikadai kuwa mumewe ndiye aliyekuwa wa kulaumiwa kwa ajali hiyo wala sio upungufu wa gari lao.