FIFA yampiga marufuku Jack Warner

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Aliyekuwa Afisa Mkuu wa Shirikisho la Kandanda Duniani, FIFA, Jack Warner, amepigwa marufuku kushiriki shughuli zo zote za kandanda maishani mwake.

Aliyekuwa Afisa Mkuu wa Shirikisho la Kandanda Duniani, FIFA, Jack Warner, amepigwa marufuku kushiriki shughuli zo zote za kandanda maishani mwake.

Kamati ya maadili ya FIFA ilisema kuwa alihusika pakubwa katika shughuli zote za kuwalipa watu pesa za shirikisho hilo kinyume cha sheria.

Uamuzi huo unatokana na jinsi shughuli za upigiji kura wa uwenyeji wa kombe la dunia la mwaka wa 2018 na 2022.

Urusi ilikabidhiwa uwenyeji wa makala yajayo ya 2018 huku Qatar ikiratibiwa kuandaa makala ya 2022 licha ya upinzani mkali.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Warner akiwa na rais wa FIFA Sepp Blatter

Bwana Warner alijiuzulu nyadhifa zake zote katika FIFA mwaka 2011 na kwa sasa anajitetea mahakamani dhidi ya mashtaka yanayotaka kuhakikisha amehamishiwa hadi Marekani iliakabiliane na mashtaka ya ufisadi dhidi yake.

Wakati huohuo, Serikali ya Uswisi imeidhinisha kuhamishwa kwa raia wa Costa Rica, Eduardo Li, hadi Marekani.

Li alikuwa mmoja wa maafisa saba wa FiFA waliotiwa mbaroni Zurich mnambo Mei usiku wa kuamkia kongamano kuu la kila mwaka la FIFA.