Kiongozi wa FDLR afungwa miaka 13 Ujerumani

Image caption Ignace Murwanashyaka

Mahakama moja ya Ujerumani imewahukumu viongozi wawili wa waasi nchini Rwanda kwa kupanga njama za kushambulia raia katika jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.

Ignace Murwanashyaka na Straton Musoni wanatuhumiwa kwa kuwaagiza wapiganaji kufanya mauaji ya halaiki pamoja na ubakaji kati ya mwaka 2008 na 2009.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wapiganaji wa FDLR

Kesi yao ilifanyika chini ya sheria ambayo inaruhusu kuwashtaki wageni kwa uhalifu ulioyafanyika nje ya taifa la Ujerumani.

Hatua hiyo ilionekana kama ushindi dhidi ya waasi waliotekeleza uhalifu nchini Rwanda.

Murwanashyaka,ambaye ni kiongozi wa kikosi cha FDLR alipewa hukumu ya miaka 13 huku Musoni ambaye ni naibu wake akihukumiwa mika 8 jela.Hatahivyo Musoni ameachiliwa huru kutokana na miaka aliyokuwa akizuiliwa.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Vita

Uwepo wa FDLR mashariki mwa Congo ni moja ya maswala yanayosababisha mizozo ya miaka nenda miaka rudi nchini humo na kusababisha vifo vya watu milioni tano katika eneo hilo.

Wawili hao waliokamatwa ,mwaka 2009 wamekuwa wakiishi nchini Ujerumani tangu mapema miaka 1990 na kutoka huko walipanga mashambulizi dhidi ya raia mashariki mwa Congo.

Walishtumiwa kwamba waliagiza mauaji ya watu kwa kukataa kushirikiana na FDLR.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption FDLR

Wakati wa kuanza wa kesi hiyo miaka minne iliopita,kiongozi wa mashtaka wa Ujerumani Christina Ritscher alisema kuwa wawili hao walikuwa wanajua kila kilichokuwa kikiendelea.