Walimu wakaidi amri ya mahakama Kenya

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mgomo wa walimu wachacha Kenya

Masomo katika shule za umma nchini Kenya yamekwama licha ya amri ya mahakama ya kuwataka walimu warejee shuleni leo Jumatatu.

Mgomo wa walimu kote nchini Kenya umeingia wiki yake ya tano.

Vyama vya walimu nchini Kenya vimesema havitatekeleza amri ya mahakama iliyowataka kusitisha mgomo huo kwa siku tisini kuanzia leo.

Image caption Walimu walikwenda mahakamani kutafuta ufafanuzi kuhusu ratiba ya mihula ambayo serikali ilibadilisha

Badala yake vyama hivyo vimerejea mahakamani leo kutaka ufafanuzi zaidi kuhusu uamuzi huo.

Hata hivyo kesi yao iliahirishwa hadi Alhamisi wiki hii.

Walimu walijitokeza kwa wingi wakiandamana na viongozi wao wa vyama vya walimu mwendo wa saa nane unusu.

Walimu walikwenda mahakamani kutafuta ufafanuzi kuhusu ratiba ya mihula ambayo serikali ilibadilisha hapo awali mgomo ulipochacha.

Haki miliki ya picha others
Image caption Walimu wamegoma wakidai serikali iwalipe nyongeza ya mishahara yao

Kesi hiyo imeahirishwa hadi alhamisi saa nane u nusu kwa sababu jaji aliyekuwa akisikiza kesi hiyo aliomba radhi iliapokee matibabu.

Jijini Nairobi hii leo shule ya Msingi ya Moi Avenue na Shule ya Msingi ya Nairobi hazikuwa na wanafunzi.

Wanafunzi wamesalia nyumbani huku walimu pia wakikosa kurejea shuleni kama walivyoagizwa na mahakama