Mchekeshaji Trevor Noah amrithi John Stewart

Haki miliki ya picha
Image caption Mchekeshaji Trevor Noah amrithi John Stewart

Msanii kutoka Afrika Kusini Trevor Noah alifungua ukurasa mpya usiku wa kuamkia leo alipoandaa shoo yake ya kwanza ya ''The Daily Show'' na kuchukua pahala pake muigizaji nguli, Jon Stewart .

Muigizaji huyo mwenye umri wa miaka 31 aliteuliwa kuandaa maonyesho ya kipindi hicho maarufu cha kuchekesha kwenye runinga ya Comedy Central.

Kwa mujibu wa tovuti inayotathmini maswala ya usanii 'Variety' raia huyo wa Afrika kusini hakuwa na msisimko.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Stewart alijiuzulu baada ya kuandaa kipindi hicho cha ''The Daily Show'' kwa miaka 16.

Deadline kwa upande wake iliandika kuwa hakuwa na cheche zozote katika shoo yake ya kwanza.

Mchambuzi wa vipindi vya runinga Brian Lowry amesema kuwa onyesho hilo lilimpa sura mpya ya kuwa mkakamavu zaidi ya hapo awali alipokuwa akitumika kama mchekeshaji aliyeigiza kama ripota.

Haki miliki ya picha n
Image caption Wachambuzi wanasema Trevor hakujaribu kuchukua pahala pa mtangulizi wake kwani nyendo zao ni tofauti

Stewart alijiuzulu baada ya kuandaa kipindi hicho cha ''The Daily Show'' kwa miaka 16.

Kwa upande wake Noah aliteuliwa kumrithi mwezi machi.

Marejeo ya kipindi hicho itakuwa leo usiku kwenye runinga ya Comedy Central at saa saba usiku wa leo.