Sunderland kumrudia Vieira?

Image caption Viera

Kilabu ya Sunderland nchini Uingereza inayokumbwa na utata kwa sasa inadaiwa kutaka kumrudia Patrick Vieira iwapo Dick Advocaat atajiuzulu.

Gazeti la MirrorSport nchini Uingereza limebaini kwamba kocha huyo anayefunza vijana katika kilabu ya Manchester City alikuwa miongoni mwa wale waliowania nafasi ya ukufunzi katika kilabu hiyo msimu uliopita na huenda wakataka usaidizi wake iwapo Advocaat ataondoka.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Dick Advocaat

Raia huyo wa Uholanzi tayari amesema kuwa atajiuzulu iwapo kocha mzuri atapatikana wakati ambapo kilabu hiyo iko chini jedwali la ligi ya Uingereza.

Sunderland inakabiliwa na hatari kubwa ya kushushwa daraja baada ya kushindwa na Manchester United siku ya Jumamosi.