Wenger:Olympiakos haina ushindani Ugiriki

Haki miliki ya picha All Sport
Image caption Wenger

Mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger anaamini kwamba Olympiakos inasaidiwa katika kampeni yake ya mechi za kilabu bingwa barani Ulaya kutokana na ukosefu wa ushindani katika ligi yao.

Olympiakos imeshinda taji la ligi ya Ugiriki mara tano huku ikishinda mechi zake zote katika ligi ya nyumbani.

''Ni timu ilio na fursa kubwa.Wanaitawala ligi yao ili kuweza kujianda kwa mashindano kama haya.,alisema Wenger''.

Arsenal imeshinda mechi zake mbili za mwisho ugenini Tottenham na Leicester.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Olympiaos ikicheza na Bayern

Lakini Wenger amekiri kuwa mechi zote mbili zilitumika kuijaribu timu hiyo.

Aliongeza kwamba :''Wakati unapoenda kucheza na Leicester na kuona ni nani anayekaa katika wachezaji wa ziada ndipo unapogundua kwamba mambo yamebadilika Uingereza.

Arsenal ilioteza mechi yao ya kwanza ya kimakundi baada ya kufungwa 2-1 ugenini Dinamo Zagreb,huku Olympiakos wakicharazwa 3-0 nyumbani na Bayern Munich.Arsenal na Olympiakos zinakutana siku ya jumanne uwanjani Emirates.