Auawa kwa kula kitoweo cha nyama India

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Nyama ya ngombe ni haramu maeneo mengi ya India ambapo Wahindu wanaamini mnyama huyo ni 'mtakatifu'.

Polisi nchini India wamewatia mbaroni watu sita baada ya mwanamume mmoja Muislamu kupigwa hadi kufa kufuatia uvumi kuwa familia yake imeficha nyama nyumbani kwao.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Watu 6 wamekamatwa na polisi nchini India baada ya kumvamia na kumpiga mwanaume mmoja hadi kufa eti alikuwa amekula nyama ya ngombe.

Mohammed Akhlaq alikokotwa kutoka nyumbani kwake Kaskazini mwa Uttar Pradesh na kushambuliwa na umati wa watu.

Mwanawe pia alijeruhiwa vibaya.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Jamaa ya muathiriwa wakiomboleza kifo chake

Kuchinja ngombe ni haramu maeneo mengi ya India ambapo wakaazi wake wengi ni Wahindu wanaoamini mnyama huyo ni mtakatifu.

Hivi majuzi Serikali ya chama cha Wahindu chenye mrengo wa kulia kimeweka sheria kali zinazopiga marufuku uchinjaji wa ngombe, uuzaji wa nyama na ulaji wake.