Kati ya Obama na Zuma nani alikosa heshima?

Image caption Kati ya Obama na Zuma nani alikosa heshima ?

Je ukimpata mtu anazungumza kwa simu utamsalimia ama utamsubiri akamilishe mazungumzo yake kisha umpe salamu zako ?

Hilo ndilo swali kuu lililoibuka kwenye mkutano wa viongozi duniani katika makao makuu ya umoja wa mataifa huko New York Marekani.

Rais wa Marekani Barack Obama alimpata rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma akizungumza kwa simu.

Rais Obama akasisitiza kumsalimia na kwa sababu moja au zaidi rais Zuma hakukata simu yake aliendelea kuzungumza na kumuacha Obama ameduwaa.

Mpiga picha mmoja alipata picha hiyo na kuiweka kwenye mtandao wa kijamii.

Image caption Je Obama alipaswa kusibiri rais Zuma akamilishe mazungumzo yake kwa sababu anamzidi umri ?

Picha hiyo imekuwa maarufu sana hasa Afrika Kusini ambapo watu wengi wanasema kuwa Obama hakuwa na adabu hata kidogo.

Kwa mujibu wa waliochangia kwenye mitandao ya kijamii Obama alipaswa kumsibiri rais Zuma akamilishe mazungumzo yake kwa sababu kiongozi huyo kutoka bara Afrika anamzidi umri.

Mjadala huo umechacha hususan baada ya gazeti la Times Live kuwauliza wasomaji wake watoe maoni yao.

Je unakubaliana nao kuwa Obama alipaswa kumsubiri Zuma akamilishe mazungumzo yake?

Toa maoni yako kwenye mtandao wetu wa Facebook na Twitter, tafuta BBCSwahili.