Burundi na Rwanda zalaumiana

Haki miliki ya picha
Image caption Paul Kagame

Taifa la Burundi limelishtumu taifa jirani la Rwanda kwa kuwafunza waasi wanaotaka Kuvuruga hali ya usalama nchini humo.

Taifa hilo limesema kuwa Rwanda inamhifadhi kiongozi wa jaribio la mapinduzi yaliotibuka mbali na kuwasaidia waasi kutekeleza mashambulizi mipakani,waziri wa maswala ya kigeni Alain Nyamitwe ameiambia BBC.

Rwanda imekana madai hayo na kusema Burundi inajaribu kupotosha watu kuhusu matatizo yake.

Haki miliki ya picha
Image caption Nkurunziza

Serikali hizo mbili zina uhusiano uliojaa hofu ,huku mataifa yote yakiwa na makabila yanayofanana.

Burundi imekumbwa na mauaji kadhaa pamoja majaribo ya mauaji tangu rais Pierre Nkurunziza ashinde uchaguzi uliokumbwa na utata mnamo mwezi Julai.