Nyani wazima kituo cha redio Zimbabwe

Image caption Nyani

Nyani wasumbufu katika kijiji cha Zvishane mjini Zimbabwe wamedaiwa kukizama kituo kimoja cha cha redio.

Mkuu wa kituo cha cha YA FM ,Munyaradzi Hwengwere, ameliambia gazeti la la serikali Chonicle kwamba kundi la nyani lilikula nyaya za fibre optic katika radio hiyo wakati wa kipindi cha asubuhi na kukilazimu kukosa kwenda hewani kwa saa moja.

''Tulibaini kwamba mnara wetu wa kurusha matangazo ambao uko juu ya mlima ulikuwa umevamiwa na nyani. Niliarifiwa kwamba kulikuwa na zaidi ya nyani watano ambao walikula nyaya hizo za kurushia matangazo.Tulipowasili katika mnara huo tuliwaona nyani hao wakitoroka'',alisema