Ubelgiji yakatiza msaada kwa Burundi

Pierre Nkurunziza Haki miliki ya picha
Image caption Ubelgiji imesema itatoa ufadhili kupitia mashirika ya misaada pekee

Ubelgiji imesema itasitisha utoaji wa ufadhili kwa miradi inayonufaisha serikali ya Burundi moja kwa moja baada ya Rais Pierre Nkurunziza kuchaguliwa kuongoza kwa muhula wa tatu, shirika la habari la Reuters limeripoti.

Mwaka 2013, Ubelgiji ilitoa msaada wa $56m (£36m) kwa Burundi, sehemu kubwa ya pesa hizo zikienda kwa serikali.

Lakini Ubelgiji inasema pesa hizo ambazo zilikusudiwa kupewa serikali sasa zitapewa mashirika ya kutoa misaada.

Muungano wa Ulaya pia umewekea vikwazo raia wane wa Burundi ambao imewatuhumu kwa “kuhujumu demokrasia”.