Walimu 245,000 kukosa mshahara Kenya

Image caption Walimu

Zaidi ya walimu 245,000 hawatapata mishahara yao mwezi huu,kufuatia mgomo wa nyongeza ya mishahara unaondelea kwa wiki ya sita sasa kulingana na gazeti la nation nchini humo.

Wengi wa wale watakaopata mishahara ni wafanyikazi wa shule ambao hawakujumuika katika mgomo huo.

Siku ya Alhamisi mahakama ya rufaa iliwagiza walimu kurudi shuleni mara moja huku ikiwa mamilioni ya watoto wa shule hawaezi kwenda shule kutokana na mgomo huo.

Mahakama ya Kenya imeiagiza serikali kuongeza mishahara ya walimu kwa hadi asilimia 50,lakini serikali inapinga hilo ikidai kwamba haina fedha za kuwalipa.