Wahamiaji 200 waingia kwa reli Ufaransa

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Wahamiaji 200 waingia kwa reli Ufaransa

Zaidi ya wahamiaji 200 wamefanikiwa kuvunja vizuizi vya usalama kwenye reli inayounganisha Uingereza na Ufaransa na kusababishwa kusimamishwa kwa huduma.

Maafisa katika mji wa bandari wa Calais nchini Ufaransa, wanasema kuwa walikabiliwa na kile walichokitaja kuwa shambulizi lililopangwa.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Wahamiaji 200 waingia kwa reli Ufaransa

Wahamiaji 100 waliingia katika reli hiyo huku wengine wakifanikiwa kuifikia reli kabisa.

Kampuni ya Eurotunnel inasema kuwa wafanyikazi walishambuliwa na wahamiaji kwa mawe ambapo watu watatu walijeruhiwa.

Mamilioni ya pauni imetumiwa kuboresha usalama katika reli hiyo, ukiwemo ujenzi wa ua mpya na kuongezwa kwa walinzi.