Soka ya Tanzania iko chini zaidi Afrika mashariki

Image caption Taifa Stars

Licha ya kupanda nafasi nne hadi nambari 136,Tanzania imeorodheshwa ya chini zaidi na shirikisho la soka duniani FIFA katika soka ya Afrika mashariki.

Kulingana na orodha ya FIFA iliotolewa siku ya Alhamisi,Uganda imeorodheshwa ya 75,ikifuatiwa na Rwanda katika nafasi ya 93.

Uganda na Rwanda zimeshuka nafasi 4 na 15 mtawalia.

Burundi nayo imerodheshwa nambari ya 113 ikiwa ya tatu ikifuatiwa na Kenya katika nafasi ya 131 ikiwa nambari 4.

Image caption Taifa Stars

Taifa Stars ya Tanzania ambayo ililazimu sare ya 0-0 dhidi ya timu ya Super Eagles kutoka Nigeria katika mechi za kufuzu kwa kombe la Afrika inashikila nafasi ya 5 na ya mwisho katika Afrika mashariki ikiwa katika nambari 136 duniani.

Kwengineko orodha hiyo mpya inaonyesha kuwa Liberia na Afrika Kusini ndizo zilizofanywa vyema.

Mataifa hayo mawili yameorodheshwa ya 95 baada ya kupanda kwa nafasi 65 na 144 baada ya kupanda kwa nafasi 54 mtawalia.

Image caption Taifa Stars

Kulingana na Shrikisho la FIFA,Ujerumani inaongoza ikifuatiwa na Argentina kisha Ubelgiji nafasi ya 3 na Ureno katika nafasi ya nne.