Blatter akataa kujiuzulu

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Blatter akataa kujiuzulu

Rais wa shirikisho la kandada duniani FIFA Sepp Blatter, amekataa wito kutoka kwa baadhi ya wafadhili wakuu wa shirikisho hilo wa kumtaka ajiuzulu mara moja.

Katika kile kinachoonekana kuwa hatua za pamoja , makampuni ya Coca-Cola, McDonald's, Visa na Budweiser, yametaka Blatter kuondoka FIFA sasa , badala ya mwezi Februari jinsi ilivyopangwa.

Visa inasema kuwa hakuna mabadiliko yoyote ya maana yanaweza kufanyika katika kipindi cha usimamizi wa sasa.

Utawala nchini uswisi unamchunguza bwana Blatter kama sehemu ya uchunguzi wake kuhusu ufisadi.