Auwawa kwa 'kula' nyama ya ng'ombe India

Haki miliki ya picha none
Image caption Auwawa kwa kula nyama ya ngombe India

Polisi nchini India wamewakamata watu wawili kuhusiana na mauaji ya mtu mmoja muislamu kutokana na uvumi kwamba familia yake imekuwa ikihifadhi na kula nyama.

Mohammad Akhlaqa alibebwa kutoka nyumbani kwake viungani mwa mji wa Delhi na kupigwa hadi kufa mapema wiki hii.

Mwanawe wa kiume pia alijeruhiwa.

Watu wanane kufikia sasa wamekamatwa kuhusiana na kisa hicho.

Familia ya bwana Akhlaq imesema kuwa ilikuwa imeweka nyama ya kondoo pekee katika jokovu.

Uchinjaji wa ng'ombe umepigwa marufuku katika majimbo mengi ya India kwa kuwa mnyama huyo huchukuliwa kuwa mtakatifu na idadi kubwa ya raia wa kihindi.

Waziri mkuu nchini India amekosolewa kwa kuwa kimya kuhusu tukio hilo.