Kanisa katoliki lamtimua askofu senge

Image caption Askofu Olaf Charamsa

Siku moja kabla mkutano wa Vatikani wa maaskofu wa kanisa Katoliki kuhusu familia, kasisi mmoja wa daraja ya juu, amedhihirisha kuwa yeye ni kati ya watu wanaopendelea uhusiano wa jinsia moja, na sasa ana mpenzi.

Msemaji wa Vatikani, alisema Kryzsztov Olaf Charamsa ambaye anatoka Poland, hawezi tena kuwa katika ofisi ya Vatikani inayotetea itikadi ya Kikatoliki.

Papa Charamsa alisema msimamo wa Kanisa hilo kuhusu jamii ya jinsia moja ni wa kizamani.

Alisema, kanisa linafaa kutambua maingiliano ya jinsia moja, na siyo kuyalaani.