Urusi yafanya mashambulizi zaidi Syria

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Syria

Ndege za Urusi zimefanya mashambulio zaidi nchini Syria.

Msemaji wa jeshi la Urusi, alieleza kuwa ndege zao zimefanya mashambulio 20 katika siku iliyopita, na kupiga maeneo kadha ya IS.

Haki miliki ya picha RIA NOVOSTI
Image caption Syria

Lakini waziri wa ulinzi wa Uingereza, Michael Fallon amesema, katika mashambulio 20 yaliyofanywa na ndege za Urusi, moja tu lililenga IS.

Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron ,amerudia tena matamshi yake ya kuikosoa Urusi akidai kuwa inaunga mkono uongozi wa rais Assad aliyemtaja kuwa muuaji.