Obama atuma rambi rambi kwa vifo Kunduz

Haki miliki ya picha
Image caption Obama atuma rambi rambi kwa vifo Kunduz

Rais wa marekani Barack Obama ametuma rambi rambi zake kwa wale waliopoteza maisha wakati wa shambulia la angani , ambapo takriban watu 19 waliuawa kwenye hospitali ya shirika la madaktari wasio na mipaka mjini Kunduz Kaskazini mwa Afghanistan.

Hata hivyo rais Obama amasema kuwa atasubiri hadi matokeo ya uchunguzi yatakapotolewa na idara ya ulinzi nchini Marekani kabla ya kutoa taarifa kamili kuhusu ni kipi kilitokea.

Haki miliki ya picha MSF
Image caption Hospitali iliyoshambuliwa Kunduz

Jeshi la Marekani lilikiri kuendesha shambulizi eneo hilo na msemaji wake alisema kuwa, walikuwa wanalenga wanamgambo na kwamba huenda kulitokea uharibifu.

Katibu mkuu wa umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametaka kufanyika uchuguzi wa kina na usiopendelea.