Watu zaidi ya 60 wauawa kwa bomu Iraq

Haki miliki ya picha AP
Image caption Gari iliyolipuliwa na Bomu nchini Iraq

Bomu lililotegwa ndani ya gari limelipuka na kuwauwa zaidi ya watu sitini nchini Iraq,katika jimbo la Mashariki la Diyala.

Bomu hilo lililenga mtaa wa kibiashara ambapo zaidi ya watu arobaini walifariki na zaidi ya hamsini kujeruhiwa.

Shambulio jingine lilitokea katika mji wa kusini mwa Basra, ambao kwa mara nyingi haukuwahi kukumbwa na milipuko nchini humo.

Maafisa mjini humo wanasema bomu hilo lilitegwa katika mtaa wa al Zubair liliwauwa watu kumi.

Kundi la Kiislamu la IS limethibitisha kuhusika katika mashambulio hayo.

Katika mji wa Baghdad polisi wamesema kuwa bomu lililotegwa ndani ya gari liliwauwa watu kumi na watatu katika kitongoji cha Husseiniya.