Ujerumani kupokea wakimbizi milioni 1.5

Haki miliki ya picha epa
Image caption Kuna shinikizo linaloongezeka la kisiasa kwa kansela wa nchi hiyo kukoma kuwapokea wakimbizi.

Wakimbizi milioni moja u nusu wanatarajiwa kutafuta hifadhi nchini Ujerumani mwaka huu kwa mujibu wa ripoti ya vyombo vya habari.

Makadirio hayo mapya ambayo hayajathibitishwa na serikali ya Ujerumani yanajiri wakati kuna ongezeko la wasiwasi kuhusu uwezo wa Ujerumani kukabilianana idadi kubwa kama hiyo ya wakimbizi na .

Serikali ya Ujerumani inakadiria watu laki nane watatafuta hifadhi huko mwaka huu licha ya kuwa baadhi ya wanasiasa wameonya huenda idadi hiyo ikaongezeka maradufu.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wasiwasi unaoongezeka kuhusu uwezo wa Ujerumani kukabiliana na hilo.

Sasa duru zilizonukuliwa katika gazeti moja la Ujerumani inadai wakimbizi na wahamiaji milioni moja na nusu watawasili mwaka huu.

Kiwango ambacho ni maradufu ya kadirio lililotolewa awali.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Ujerumani kupokea wakimbizi milioni 1.5

Wasiwasi unaoongezeka kuhusu uwezo wa Ujerumani kukabiliana na hilo.

Jana maelfu ya watu walijumuika katika maandamano ya kupinga wakimbizi katika baadhi ya miji Ujerumani.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Serikali ya Ujerumani inakadiria watu laki nane watatafuta hifadhi huko

Na kuna shinikizo linaloongezeka la kisiasa kwa kansela wa nchi hiyo kukoma kuwapokea wakimbizi.

Lakini, Angela Merkel anaendelea kutetea sera yake ya kuruhusu wakimbizi hao akisisitiza nchi hiyo ina uwezo wa kukabiliana na hali iliyopo.