Ulaya kufadhili kambi za wahamiaji Uturuki

Haki miliki ya picha
Image caption Uturuki ni moja ya njia kuu ambayo maelfu ya wahamiaji hutumia kuingia Ulaya.

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan, yuko mjini Brussels kwa mazungumzo muhimu na viongozi wa muungano wa bara Ulaya, kuhusu suala la uhamiaji.

Kuna takriban wakimbizi milioni 2 wa Syria nchini Uturuki.

Nchi hiyo ni moja ya njia kuu ambayo maelfu ya wahamiaji hutumia kuingia Ulaya.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Ulaya, ina matumaini ya kuafikia makubaliano kuhakikisha kuwa wahamiaji na wakimbizi zaidi wanabakia nchini Uturuki.

Viongozi wa muungano wa bara Ulaya, wana matumaini ya kuafikia makubaliano kuhakikisha kuwa wahamiaji na wakimbizi zaidi wanabakia nchini Uturuki.

Pia wanatarajiwa kukubaliana kuhusu doria za pamoja katika pwani ya Uturuki

Awali, Uturuki ilisema kwamba ilituma ndege zake mbili za kijeshi aina ya F-16 kuzuia ndege ya kijeshi ya Urusi iliyokuwa imeingia katika anga yake bila ruhusa Jumamosi.

Ndege hiyo ya Urusi "iliondoka anga ya Uturuki na kuingia" Syria baada ya kuzuiwa, wizara ya mashauri ya kigeni ya Uturuki imesema.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Ulaya inapania kufadhili kambi za wahamiaji Uturuki ilikuzuia wakimbizi zaidi kutoenda ulaya

Waziri wa mashauri ya kigeni wa Uturuki amezungumza na mwenzake wa Urusi, pamoja na mawaziri wengine kutoka kwa shirika la kujihami la Nato.

Uturuki imesema ilizuia ndege hiyo ya Urusi katika eneo lililo kusini mwa jimbo la Yayladagi/Hatay.

Wizara ya mashauri ya kigeni mjini Ankara ilimwita balozi wa Urusi nchini humo "kulalamika vikali" kuhusu kisa hicho.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Awali, Uturuki ilisema kwamba ilituma ndege zake mbili za kijeshi aina ya F-16 kuzuia ndege ya kijeshi ya Urusi iliyokuwa imeingia katika anga yake bila ruhusa Jumamosi.

Russia imekuwa ikitekeleza mashambulio ya angani nchini Syria, dhidi ya wapinzani wa Rais Bashar al-Assad.

Mashambulio hayo yalianza Jumatano wiki iliyopita, Urusi ikisisitiza kwamba inalenga tu maneneo yanayodhibitiwa na kundi la Islamic State.

Lakini wanaharakati wa kutetea haki nchini Syria wanasema ndege za Urusi pia zilishambulia makundi mengine yanayompinga Rais Assad.

Wiki iliyopita, Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan alitaja hatua ya Urusi kuingilia mzozo nchini Syria kama "kosa kubwa" ambalo litapeleekea kutengwa zaidi kwa Moscow.