Boko Haram wasema wanatii Islamic State

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Bendera ya Boko Haram inafanana kama ile ya kundi la islamic state

Kundi la Boko Haram nchini Nigeria limetoa kanda ya video inayothibitisha utiifu wao kwa kundi la Islamic State.

Msemaji asiyejulikana amesisitiza kuwa kundi hilo liko chini ya ongozi wa Abubakr Shekau.

Hatahihivyo Shekua hajaonyeshwa katika kanda hizo za video na kuzua uvumi kwamba huenda ameuawa ama kumalizwa nguvu.

Msemaji huyo vilevile amekana madai ya hivi karibuni ya jeshi la Nigeria kwamba wanachama wa kundi la Boko Haram wamesalimu amri na kusema kuwa jeshi limeshindwa katika vita.