Facebook kuanzisha Satelite YAO

Haki miliki ya picha Facebook
Image caption Satelite ya Facebook

Kampuni ya Facebook imetangaza kuwa itaanzisha mtandao wa satelite ili kutoa huduma za internet kwenye maeneo yaliyo mashambani barani Afrika.

Kwa ushirikiano na kampuni ya Eutelsat, iliyo Ufaransa, Facebook wanatumainia kuwa mtambo wa kwanza wa satelite utakuwa tayari kuzinduliwa mwaka ujao. Baadhi ya mataifa, kama India yanapinga hatua hiyo ya Facebook, ambayo wanadai inahujumu kampuni ndogo zinazotoa huduma za simu katika mataifa yanayoendelea.