Katanga aiomba ICC imwachilie huru

Germain Katanga Haki miliki ya picha ICC
Image caption Katanga amekaa gerezani miaka minane

Mbabe wa kivita kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Germain Katanga, ameiomba mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita (ICC) imwachilie huru.

Katanga alifungwa jela baada ya kupatikana na hatia kuhusiana na shambulio kwenye kijiji kimoja mashariki mwa DR Congo.

Ahukumiwa kifungo cha miaka 12 gerezani miezi 18 iliyopita lakini ikizingatiwa kwamba amekaa gerezani miaka minane, ukiongeza muda aliokaa rumande, ana haki ya kuomba kuachiliwa kwa mujibu wa sharia za ICC.

Wakati wa kuwasilisha ombi lake, Katanga aliomba radhi waathiriwa wa vitendo vyake na kusema amesikia “vilio vyao vya uchungu na mahangaiko kwa majuto makubwa,” shirika la habari la AFP limeripoti.